The House of Favourite Newspapers

Baada ya kupigwa na Kupaza…Muumini adaiwa kumtapeli Kinyaiya

1

1-001

Mkurugenzi wa Bendi ya Double M Plus, Muumin Mwinjuma

GLADNESS MALLYA

BAADA ya sakata la kupigwa ngumi na mwanamuziki wake, Salehe Kupaza, Mkurugenzi wa Bendi ya Double M Plus, Muumin Mwinjuma anadaiwa kumtapeli mtangazaji wa Channel Ten, Benny Kinyaiya.

Chanzo makini kililieleza gazeti hili kuwa siku ya uzinduzi wa bendi yake uliofanyika katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, Muumin alimpa kazi ya ushehereshaji ‘U-MC’ wa shughuli hiyo Kinyaiya ambayo aliifanya kwa ufasaha mpaka mwisho huku wakikubaliana kwamba atampa fedha ya mafuta ya gari shilingi laki moja na nusu lakini baada ya hapo mkurugenzi huyo aliingia mitini bila kumlipa chochote.

8

Salehe Kupaza

“Yaani huyu Muumin ni mdhulumati kwani ameingia mitini na hela ya U-MC ya Kinyaiya na kila akimtumia meseji hamjibu chochote na hakumpa hata shilingi baada ya uzinduzi kuisha aliondoka zake mpaka leo yupo kimya, inamuuma sana Kinyaiya ila ameamua kumwachia Mungu,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, Amani lilimtafuta Kinyaiya ambaye alikiri kwamba ni kweli ilitokea ila ameamua kumsamehe.

5

Mtangazaji wa Channel Ten, Benny Kinyaiya.

“Jamani mmeyajuaje hayo? Ni kweli tulielewana atanipa hela ya mafuta lakini mpaka leo yupo kimya nami nimeamua tu kumsamehe,” alisema Kinyaiya.

Kwa upande wa Muumin alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikuwa na haya ya kusema;

“Siyo kweli kwamba ananidai laki moja na nusu ni hivi, tulikubaliana nitampa laki moja lakini fedha ziliisha nikamwambia nitampa ila nitamlipa tu maana uzinduzi siyo kazi rahisi ndiyo maana nilikuwa nataka MC awe Mwanahawa Chipolopolo ili kupunguza gharama lakini Kupaza akasema tumchukue huyo Kinyaiya yupo tu.”

1 Comment
  1. […] mwa marapa wa kike wanaofanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Chemical ni miongoni mwao ambapo hivi […]

Leave A Reply