

GARETH BALE ameendelea kufunga mabao mara sita mfululizo wakati timu yake ya Real Madrid ilipoibamiza Girona, akiendelea kuonyesha kwamba bado timu hiyo iko ngangari hata baada ya kuondoka kwa nyota Cristiano Ronaldo.
Mchezaji huyo alifunga mabao mawili ambapo Sergio Ramos na Karim Benzema walifunga mabao mawili kwa njia ya penalti.
Juhudi hizo za Bale zilimfanya hadi jana kufikisha mabao 150 katika ulimwengu wa soka.




