
Khloé Kardashian alipokuwa mjamzito.
PAMOJA na kwamba bado ni kibinti kidogo, True Thompson, kitoto cha nyota Mmarekani, Khloé Kardashian, bado kinapata maraha na mastarehe yote yaliyozagaa katika familia maarufu ya Kardashian ya nchini humo.
Miongoni mwa ‘shopping’ kaliyofanyiwa majuzi ni kununuliwa kigari halisi kidogo aina ya Bentley na mazagazaga mengi yaliyoongozwa na mama wa familia hiyo maarufu aitwaye Kris Jenner.

Mipango ya chereko kabla ya kuzaliwa kwa True ilianza mapema na ikaendelea hadi majuzi kigari hicho kiliponunuliwa kwa bei kubwa ambapo gharama ya chereko hizo ilikuwa zaidi ya Dola 90,000 (Sh. mil. 205).