Beki Mtaalamu Simba Awatumia Salamu Yanga

HARUNA Shamte, beki mpya ndani ya Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili amesema kuwa moto wake haupoi msimu ujao ataendelea kuwaliza wapinzani wa Simba ikiwa ni pamoja na Yanga.

 

Shamte akiwa ndani ya Lipuli, alipachika jumla ya mabao 5 yote kwa mipira iliyokufa ambapo kati ya hayo matatu ilikuwa ni kwenye Kombe la Shirikisho na mawili kwenye Ligi Kuu Bara.

 

“Nimetua Simba kwa ajili ya kuendeleza kazi yangu ambayo ni mpira hivyo wapinzani wetu wajipange kwani kikosi chetu ni imara na kipo tayari kuleta ushindani.

 

“Msimu uliopita ulikuwa bora kwangu na niliwapachika mabao wengi hasa kwa mipira iliyokufa kutokana na kufanya mazoezi, hivyo bado naendelea kufanya mazoezi ili kuwa bora zaidi kwa ajili ya mechi zote” alisema Shamte.


Loading...

Toa comment