Mkazi wa Tanga Bi. Agness Lymo (54) ameibuka mshindi wa pikipiki katika droo ndogo iliyochezeshwa leo Jumatano kwenye Viwanja vya Bakhresa jijini Dar.
Katika droo hiyo kuelekea droo kubwa ya mchezo wa kubahatisha kujishindia nyumba, washindi wanne walipatikana ambapo mshereheshaji wa hafla hiyo, Chaku Shemungia alianza kuwataja washindi hao ambapo kuponi zao ziliibuka kidedea katika droo hiyo.
Katika droo hiyo alianza kutafutwa mshindi wanne ambapo baada ya kuponi hizo kuchanganywa mbele ya umati uliofurika uwanjani hapo, kuponi ya Eveline Thomas wa Keko jijini Dar ilishinda na hivyo kutangazwa kuwa mshindi wa seti ya vyombo (Dinner set).
Mshindi wa tatu alikuwa Shaban Muhindila (66) wa Morogoro aliyeibuka na tivii bapa (Flat screen).
Mashuhuda waliokuwa uwanjani hapo viroho vikiwadunga kumtaka kumjua mshindi wa pili kuponi ya Mgaza Mwemanga (56) mkazi wa Manzese jijini Dar ndiyo iliyoibuliwa ambapo ziliibuka shangwe na nderemo uwanjani hapo ambapo mshindi huyo na ndugu na jamaa zake walikuwepo kwenye viwanjani hapo.
Mgaza alijishindia simu ya kisasa aina ya Phantom 6.
Kutokana na furaha aliyokuwa nayo Mgaza ilibidi mshereheshaji Mc Chaku ampe kazi ya kuchanganya kuponi na kuichagua kuponi ya mshindi wa kwanza.
Mgaza ambaye alijinadi kuwa yeye ni msomaji mkubwa wa magazeti ya championi na Risasi aliufanya mchakato huyo ambapo bahati ya mshindi wa kwanza ilikwenda kwa Bi. Agnes Lymo (54) mkazi wa Tanga na kuhitimisha zoezi hilo.
Katika tukio hilo sambamba na Global ilishirikiana kiukaribu kukamilisha mchakato ikiwa na British School, Kampuni ya Ving’amuzi vya Ting, Tecno Exprience More na wengineo.
Sambamba na washindi hao wengine walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo fulana, kalenda za British School nk.
(PICHA/ HABARI: RICHARD BUKOS/GPL)
[…] wa Tanga Bi. Agness Lymo (54) ameibuka mshindi wa pikipiki katika droo ndogo ya tatu ya Shinda Nyumba iliyochezeshwa jana Jumatano kwenye Viwanja vya Bakhresa jijini […]
[…] wajukuu wanne, umri wake ni miaka 70, na kila mmoja hushangazwa na muonekano wake! Ni bibi asiye mzee. Ajabu […]