BINTI HUYU ANASIKITISHA, APATA GONJWA ATIMULIWA KWAO

Joyce Joseph akiweka pozi.

 

INAUMA sana. binti mmoja mmoja aliyejulikana kwa jina la Joyce Joseph (18), mkazi wa magu mkoani mwanza, yuko kwenye kipindi kigumu cha mateso na maumivu ya ugonjwa wa kansa ya ngozi huku akiwa ametimuliwa katika nyumba aliyokuwa anaishi.

 

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Joyce alianza kusimulia historia yake ya maisha kwa kusema, awali alikuwa akiishi kama mmoja wa watoto katika familia ya mama Mayeji lakini baadaye alianza kunyanyaswa baada ya kuanza kuumwa.

 

Ngozi ilivyodhurika.

“Mimi niliokotwa nikiwa mtoto mdogo wa siku mbili ambapo mama huyu niliyekuwa naishi naye alikuwa akienda kuuza nyanya sokoni akanikuta nimetupwa kwenye mfuko wa rambo ndipo aliponiokota na kuanza kunilea kama mtoto wake bila mimi kutambua chochote,” alisema Joyce.

Akisimulia zaidi kwa uchungu, alisema baadaye alikuja kugundua kuwa si mtoto wa familia hiyo pindi alipoanza kuugua ugonjwa wa kansa akiwa na umri wa miaka 10.

Nywele na shingo vilivyoathirika.

Alisema alipoanza kuugua, alianza kutokwa na vipele kama ugonjwa wa tete kuwanga mwilini ambapo alianza kujikuna kila mara na vipele hivyo vikawa haviponi. “Yaani nilikuwa najikuna kweli mwili mzima lakini cha ajabu kila nilipokuwa nikivipasua vipele hivyo, vililikuwa haviponi jambo ambalo lilinifanya nihisi kuwa nina tatizo mwilini,” alisema Joyce.

Binti huyo alisema mama huyo alikuwa akijaribu kumpeleka katika hospitali mbalimbali kutafuta tiba lakini kila alikoenda, hakupata tiba sahihi lakini kilichomuuma zaidi, baba wa familia hiyo akaanza kumnyanyapaa kwa kumpiga na kumtenga na watoto wengine. “Niliumia sana. Baba badala ya kumsaidia mama, akaanza kuninyanyapaa.

 

Joyce akiweka pozi.

 

Hapo ndipo nilipojua sasa kumbe mimi si mtoto wa familia hiyo baada ya baba kuanza kunipiga kila mara bila kosa lolote na kutufukuza mimi na mama mpaka kufikia hatua ya kumvunja mkono mama na kumwambia kuwa anahangaika na mimi wakati siyo mtoto wake,” alisema Joyce.

 

Joyce aliendelea kuzungumza kuwa, mama huyo aliendelea kuhangaika naye wakati mwingine naye akawa anampiga na kujikuta akikosa msaada hivyo kuamua kutoweka nyumbani hapo na kuanza kuwa analala mitaani mpaka alipokutana na msamaria mmoja aliyemshauri kwenda kuonana na Flora Lauo kupitia taasisi yake ya Nitetee ambaye ndiye aliyegundua kuwa ana tatizo la kansa ya ngozi.

Akiwa na familia yake.

 

“Nilikutana na msamaria mmoja ndiyo akanishauri niende kwa Flora Lauo. Nashukuru Mungu alinipokea, na ndipo nilipopima na kugundulika kuwa nina kansa ya ngozi, nimeanza matibabu katika Hospitali ya Bugando lakini kiukweli bado nahitaji fedha kwa ajili ya matibabu,” alisema Joyce.

 

Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la Joyce, tafadhali anaombwa kumchangia chochote alichonacho ili aweze kuendelea na matibabu zaidi kupitia simu yake ya mkononi; 0752 675883.

 

STORI: IMELDA MTEMA| RISASI JUMAMOSI| DAR ES SALAAM

Loading...

Toa comment