The House of Favourite Newspapers

Bocco, Manula Wachunia mikataba Simba

 

MASTAA watatu tegemeo wa Simba wakiongozwa na nahodha, John Bocco, beki kiraka Erasto Nyoni na kipa, Aishi Manula wamegoma kusaini mikataba mipya. Wachezaji hao waliojiunga Simba wakitokea Azam FC ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika mwishoni mwa msimu huu. Wengine baadhi ni Shomari Kapombe, Juuko Murshid, Emmanuel Okwi, James Kotei Nicholas Gyan na Asante Kwasi.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, nyota hao wamegomea mikataba hiyo kutokana na kushindwana kwenye maslahi. Mtoa taarifa huyo alisema, bado mazungumzo yanaendelea kufanyika kati ya wachezaji hao na viongozi wa timu hiyo ili kuhakikisha wanaendelea kukipiga Simba katika msimu ujao.

 

“Kama mazungumzo hayatakwenda vizuri kati yao, basi upo uwezekano wa wachezaji hao wasisaini mikataba mipya.

”Na kikubwa kinachokwamisha hilo ni suala la dau la usajili walilowekewa mezani ambalo wao hawakubaliani nalo, ni dogo, hivyo wameomba waongezwe kabla ya kusaini mkataba huo,” alisema mtoa taarifa huyo. Alipotafutwa Mkurugenzi Mtendaji (C.E.O) wa Simba, Cresncetius Magori kuzungumzia usajili huo, alisema: “Tumepokea mapendekezo kadhaa ya usajili kutoka kwa kocha wetu Aussems (Patrick) kati ya hao wapo tutakaowaongezea mikataba, tutakaowatoa kwa mkopo na wale tutakaowaacha kabisa. “Hivyo, sitaweza kulizungumzia hilo la akina Bocco na kiukweli bado hawajasaini mikataba mipya, kilichokwamisha ni mchezo wetu wa mwisho dhidi ya ligi na Mtibwa Sugar.”

Mbowe, Ester Matiko Walivyowasili Kisutu Kusikiliza Kesi Inayowakabili

Comments are closed.