The House of Favourite Newspapers

BONGE LA NYAU ATOBOA SIRI YA KUPOTEA KWENYE GEMU

0
Hii ni moja ya picha y Bonge la Nyau ikliyokwenye Video yake

 

Baada ya kupotea kwenye gemu kwa zaidi ya mwaka mzima, msanii wa Bongo Fleva , Bonge la Nyau, amefunguka kwamba malezi ya mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni ndiyo yaliyomfanya akaupa kisogo muziki.

Bonge la Nyau ambaye kwa sasa ametoka na ngoma mpya iitwayo Homa ya Mapenzi, aliyomshirikisha Barakah The Prince, amesema Mungu amemjaalia kupata mtoto wa kike aitwaye Malaika aliyemfanya aamue kugeukia mambo ya kifamilia kwa muda.

“Sikukaa kimya kihivyo, ni mwaka mmoja tu, nilikuwa bize na majukumu mengine kwani hapa katikati namshukuru Mungu nilifanikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Malaika, kwa hiyo familia na mambo mengine ya kimaisha yakanifanya nikae kimya kwa muda,” alisema Bonge la Nyau.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply