The House of Favourite Newspapers

Heshima ya Bongo Fleva…Wakongwe 15 Kupigwa Mizinga leo Dar Live

2
Staa Mkongwe, Prince Dully Sykes.

BAADA ya kusubiriwa kwa hamu na mashabiki na wadau wa burudani, hatimaye ile siku imefika ambapo leo (Julai Mosi) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, wakongwe zaidi ya 15 kunako Muziki wa Bongo Fleva watapigiwa mizinga ya heshima.

Mashabiki wakiwa katika shoo ya Nishushe Dar Live iliyofanyika hivi karibuni.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mkuu wa Masoko wa EATV, Roy Mbowe alisema kuwa, Heshima ya Bongo Fleva ni sehemu ya kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na huwa kinatambulika hivyohivyo yaani Heshima ya Bongo Fleva ambapo huchezwa miziki ya zamani tu na stori za zamani za muziki huo pamoja na kufanya mahojiano ya live na wadau na wasanii wa zamani.

Msanii wa Bongo T.I.D Mnyama.

“Katika tamasha hili, tumewajumuisha wakali wote kwa dhumuni la kutambua mchango wao katika muziki wa zamani. Hivyo basi tutakuwa na vichwa vya zamani zaidi ya 15 vilivyobambana vinavyoendelea kusumbua katika muziki huu vikigonga nyimbo zote za zamani tu. Mashabiki mjitokeze kwa wingi kushuhudia tukio hili ambalo ni la kwanza katika historia ya Muziki wa Bongo Fleva,” alisema Roy.

WATAKAOPAFUMU SASA!

Roy alitaja listi ya wakali hao watakaokinukisha leo kuwa ni T.I.D Mnyama atakayetikisa na ngoma kibao ikiwemo Zeze , Watasema na Rahisa, Juma Nature atawakumbusha ngoma zote akiwa na Wachuja Nafaka, TMK Wanaume Halisi huku Q Chillah akiwakumbusha mashabiki kwa ngoma yake ya Zamani (Nikilala Naota), Mariamu, Zaidi ya Jana na nyinginezo.

Mkongwe wa Muziki wa Bongo, Juma Nature.

“Wakali kama Mandojo na Domokaya nao watafufukia Dar Live huku naye MB Dog akiwakilisha na ngoma zake za zamani kama vile Latifa na Natamani. Wengine ni Prince Dully Sykes akiwa na ngoma zake kibao za zamani kuanzia Julieta, Salome na Leah, pia tutakuwa na mzee wa Mwanangu Huna Nidhamu, Dudu Baya pamoja na mkali aliyekuwa akiunda kundi la Daz Nundaz, Daz Baba,” alisema Roy na kuongeza;

“Wengine tutakaokuwa nao ni mkali wa ngoma ya Binti Kiziwi na Mpenzi Jini, Z-Anto, makundi yaliokuwa tishio zamani kama vile Wagosi Wakaya, Mabaga Fresh na Solid Ground Family.”

KIINGILIO JE?

Roy alimalizia kwa kutaja kuwa shoo nzima itakwenda kwa mtonyo kiduchu tu.

“Pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia saa 2:00 za usiku kwa kiingilio kidogo tu cha shilingi 7,000 tu.”

Tamasha la Heshima ya Bongo Fleva limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Uwazi

2 Comments
  1. […] ya kufanya vizuri na baadhi ya ngoma zake kama Na Yule, Sijutii, na nyingine nyingi, staa wa Bongo Fleva, Ruby, amemuanika baba kijacho wake kwenye ukurasa wake wa […]

  2. […] ya kupotea kwenye gemu kwa zaidi ya mwaka mzima, msanii wa Bongo Fleva , Bonge la Nyau, amefunguka kwamba malezi ya mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni ndiyo […]

Leave A Reply