The House of Favourite Newspapers

Bongo Fleva Kupaa Kenya Kushiriki Mkutano wa Wasanii

1
Mwenyekiti wa Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya, Samwel Mbwana (wa kwanza kulia, mwanamuzki Stala Thomas).

 

BAADHI ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini wanatarajia kwenda nchini Kenya kushiriki mkutano ulioandaliwa na ajili ya kutoa elimu kwa wasanii, mkutano utakaofanyika kuanzia Julai 3 hadi 6 mwaka huu.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya, Samwel Mbwana amesema kuwa lengo kubwa la mkutano huo ni kuzungumzia masuala ya kimuziki.

Chama cha Wanamuziki Tanzania (TUMA) kimewataka wasanii nchini kujitokeza kujisajili katika Chama hicho ili waweze kupata fursa za viwango vya sanaa na kujifunza kwa wenzao wa nchi nyingine.

 

 

Bw.  Mbwana amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa fursa ya sanaa kwa wasanii wameona ni vema kuzunguka nchini ili kutoa elimu juu ya suala hilo.

Aidha amesema kuwa tayari wameanza ziara hiyo katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Mbeya ambako tayari wametoa elimu kwa wasanii ili wawe na maadili mema katika sanaa zao.

Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bw.Godfrey Mungereza akizungumza na wanahabari

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bw.Godfrey Mungereza amewapongeza kwa kuweka umoja huo na kusema Basata inaunga mkono juhudi hizo zitakazowasaidia kutetea maslahi ya wanamuziki wote

PICHA ZOTE NA DENIS MTIMA | GLOBAL TV ONLINE

1 Comment
  1. […] wa Bongo Fleva, Abdu Kiba, ameibuka na kuwatolea uvivu wale wote wanaosema kwamba kaka yake, Ally Kiba, amefulia […]

Leave A Reply