The House of Favourite Newspapers

Bosi mpya ambakiza Ajibu Yanga

KUELEKEA kipindi cha usajili, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amefunguka kuwa mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu atabaki Yanga, suala la kuondoka ni uamuzi wake.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa za nyota huyo kusaini mkataba wa awali Simba kwa ajili ya msimu ujao. Ajibu alijiunga na Yanga msimu wa 2017/18 akitokea Simba ambapo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Msolla alisema kuwa lengo lao ni kumbakisha Ajibu pamoja na wale wachezaji ambao benchi la ufundi litahitaji kufanya nao kazi kwa msimu ujao. Msolla alisema kipindi cha usajili kikifi ka kocha ndiye mwenye maamuzi ya mwisho wa kuamua ni mchezaji gani ambaye atabaki katika kikosi hicho.

 

“Ajibu ni mchezaji wetu na malengo ni kuendelea kubaki hapa Yanga ndiyo maana tunatafuta fedha kwa bidii kuona wachezaji wetu wanakuwa imara msimu ujao ingawa ni uamuzi wake kuondoka na lazima ajipime na kujitafakari mwenyewe.

 

“Tunapambana kuona msimu ujao tunakuwa na wachezaji ambao watakuwa imara na kutengeneza timu yenye ushindani katika ligi pamoja na kimataifa ndiyo maana tutamsikiliza mwalimu,” alisema.

 

Ajibu mpaka sasa msimu huu amefanikiwa kufanga mabao sita huku akitoa asisti 17 katika mabao 55 ambayo yamefungwa na kikosi hicho kwenye mechi 36 na wakiruhusu mabao 25.

Martha Mboma na Khadija Mngwai

 

UCHAMBUZI: Mwalimu KASHASHA “Simba Wanacheza Mpira wa Majukwaa”

Comments are closed.