Bosi mpya: Usajili wa Simba Utakuwa wa Kisomi

OFISA Mtendaji Mkuu mpya wa Simba, Senzo Mazingiza raia wa Afrika Kusini, ameweka wazi kuwa atahakikisha klabu hiyo inafanya usajili wa kisomi katika dirisha dogo Desemba ambao utaibeba timu hiyo kwenye harakati zake za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

 

Mazingiza amekwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wenzake saba aliokuwa ameomba nao ambapo anachukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye amemaliza muda wake.

 

Bosi huyo amesema kwamba atahakikisha anasimamia vizuri suala la usajili ndani ya kikosi hicho na kuwaleta wachezaji ambao watakuwa na viwango vikubwa.“Najua Simba ni timu kubwa na yenye malengo mapana, sasa ni lazima mambo yaende kiuwazi wa juu na kisomi pia.

 

“Najua kunahitajika nguvu kubwa ya wachezaji ambao wataisaidia timu kwenye ligi, hasa baada ya kuondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Nitasimamia suala la usajili kuona Simba inapata wachezaji wa juu ambao watakuwa na uwezo wa kuichezea timu, kuhakikisha kuwa inatwaa ubingwa wa ligi kwa mara nyingine tena,” alisema Msauz huyo.

IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment