The House of Favourite Newspapers

BREAKING: CHADEMA WAJIONDOA CHAGUZI NDOGO ZOTE

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kujiondoa katika chaguzi ndogo zote zilizotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na zitakazofuata kikisema tume hiyo inafanya kazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe. aliposema NEC inafanya kazi ya kuhakikisha chama tawala chini ya Rais John Pombe Magufuli kinashinda kwa kulazimisha matokeo.

 

Mbowe amesema hawatashiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Liwale na kata 37 kwa kile alisema kuwepo mazingira magumu ya kisiasa na kiuchaguzi.

 

“Ukonga kulikuwa na vituo feki 16 vyenye wapiga kura zaidi ya 7,000 na viliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuongeza kura za CCM. Tulipeleka malalamiko yetu NEC na kwa Msimamizi wa Uchaguzi, lakini hakuna kilichofayika.

 

“Upole na ukimya wa vyama vya upinzani hauashirii woga hata kidogo, yale mawazo ya wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi kuamini wana dola na ndiyo wenye nguvu ni kujidanganya, hakuna jeshi linaloweza kuwa na nguvu kuwazidi raia wa Tanzania.

 

“Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa vikitembea na viongozi wake CCM na vimeacha kushughulika na matukio ya kijamii, hata Bunge lililokatazwa kuonyeshwa mubashara kwa kisingizio cha kusema watu wafanye kazi, lakini rais anatembea na (shirika la utangazaji la serikali) TBC watu wakiwa makazini pia,” amesema Mbowe.

Comments are closed.