visa

BWANA WA ZARI AMFANYIA KUFURU TIFFAH!

DAR ES SALAAM: Juzi Jumanne (Agosti 6, 2019), binti wa staa wa Afro- Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ aliangushiwa bonge la pati ya siku yake ya kuzaliwa (birthday).  Tiffah alikuwa akitimiza umri wa miaka minne, shughuli ambayo ilijaa vijembe vya kila aina kwa baba’ke, Diamond au Mondi kutoka kwa Team Zari.

KING BAE AFANYA KUFURU

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uganda, mwanaume mpya wa Zari almaarufu King Bae, ameamua kutumia tukio hilo kummaliza Mondi kwa kumfanyia Tiffah kufuru ya aina yake.

Kwa mara nyingine mwaka huu, Mondi ameshindwa kuungana na Tiffah kwenye siku hiyo muhimu ya kuzaliwa kwake akiwa ndiye uzao wake wa kwanza hapa duniani. Gazeti la Amani linafahamu kuwa, wakati shughuli hiyo ya Tiffah ikifanyika huko Pretoria, Afrika Kusini (Sauz), Mondi alikuwa kwenye shoo New York nchini Marekani.

KUMBUKUMBU ISIYOFUTIKA

Ikumbukwe kuwa, shughuli hiyo inakumbusha tukio kama hilo la mwaka jana ambapo kwa mara ya kwanza Mondi alishindwa kuhudhuria au kumfanyia shughuli mwanaye huyo wakati ilikuwa ni miezi kadhaa tangu alipotengana na Zari. Zari na Mondi waliachana rasmi Februari 14, 2018, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day).

KING BAE APANIA

Imeelezwa kuwa King Bae anaonekana wazi aliipania siku hiyo baada ya kudaiwa kuandaa watu maalum wa kumpiga picha mbalimbali Tiffah akiwa amevalia kama bibi harusi na nyingine akiwa na rundo la zawadi yakiwemo magari makali ya watoto.

“Kwa kweli King Bae ni kiboko, vitu vyote hivyo ni kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa tu ya mtoto wa mwanaume mwenza? “Huu ni ujumbe tosha kwa Baba Tee (Mondi) kwamba kuna wanaume wanajua kujali familia hata kama wake zao wamezaa na wanaume wengine,” ilisomeka sehemu ya habari hizo kwenye mitandao ya Uganda.

TIFFAH ASHANGAZA

Watu kutoka kona mbalimbali walionesha kushangazwa na namna ambavyo Tiffah amekuwa haraka ambapo kwa sasa anaonekana binti mkubwa. “Angalia hata kuvaa kwake magauni yenye mishono ya wadada wakubwa, anavyobana nywele na mapochi yake ya Cucci, ni kama masistaduu ya mjini,” ilisomeka sehemu ya maoni katika picha za Tiffah.

VIJEMBE KILA KONA

Kufuatia tukio hilo, vijembe kutoka Team Zari vimeendelea kutawala kwa Mondi kwenye mitandao ya kijamii kuwa analelewa wanaye na mwanaume mwingine.

Hata hivyo, wengi kati ya waliotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kitendo cha King Bae kumfanyia Tiffah bethidei walisema inawezekana jamaa huyo alifanya hivyo kwa maelekezo ya Zari ambaye ametengana na Mondi kama sehemu ya kumuonesha jamaa huyo kwamba kuna watu wanajua kujali familia zao.

MONDI AMUOMBEA KWA MUNGU

Katikati ya maneno mengi, Mondi alimpongeza Tiffah anayetimiza miaka minne akimtakia maisha marefu na kumuombea Mungu ampe akili, afya njema na adabu.

Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye kipengele cha Insta Story aliandika; “I do love you, not because you are my daughter… Nah! I love you because you love me more than anything in the world… Sometimes I even wonder why you love me so…. and that is the reason why I can’t sleep without praying for you..

“I can’t sleep without thinking about you…and most of the time when you come to my mind, I feel like i owe you more than a life… Inshaallah, Mwenyezi Mungu akukuze vyema, akupe akili, afya, adabu, umri mrefu wenye furaha na future nzuri baadae….

“Nakupenda sana mwanangu, nakupenda sana Tiffah wangu… Happy 3 Birthday mama @princess_ tiffah.”

AKOSOLEWA KUHUSU UMRI

Hata hivyo, baada ya kuandika ujumbe huo, baadhi ya watu walimkosoa Mondi kwamba alikosema umri wa mwanaye huyo kwa kusema ana umri wa miaka mitatu badala ya miaka minne. “Unaona sasa, tukisema hajui kulea mnasema tunamuonea, ona sasa anakosea hata umri wa mwanaye,” aliandika mmoja wa Team Zari.

TULIKOTOKA

Tiffah alizaliwa Agosti 6, 2015 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar. Mbali na Tiffah, mwaka mmoja baadaye, wawili hao walijaaliwa mtoto wa kiume aitwaye Prince Nillan. Tangu wawili hao walipotengana, Mondi amekuwa akilalama kuwa Zari amekuwa akimnyima kuwaona wanaye
Toa comment