The House of Favourite Newspapers

CCM Yamnasua Mashinji Jela, Yamlipia Mil. 30 – Video

0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam,  kupitia  Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa,    Humphrey Polepole, leo Machi 11, 2020, kimemwepusha kwenda jela miezi mitano Vincent Mashinji  kwa kumlipia Sh. mil. 30 za hukumu iliyotolewa dhidi yake na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  baada ya kutiwa hatiani katika kesi iliyomhusisha yeye na viongozi wengine saba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyotolewa jana.

 

”Kulikuwa na mchakato wa ndani … na asubuhi ya leo tumekuja hapa mahakamani kupata utaratibu wa namna tunavyoweza kumnusuru ndugu yetu Vincent Mashinji,”  alisema Polepole akizungumza na waandishi mahakamani Kisutu.

 

Naye mkewe Mashinji aitwaye, Happy, alisema baada ya mumewe kulipiwa faini hiyo: “Kama familia hatukutegemea mambo yataenda haraka namna hii… kwa sababu kama mnavyojua, Vincent ni mwanachama mpya…”

POLEPOLE AIBUKA MAHAKAMANI KUMLIPIA FAINI DKT MASHINJI ATOKE GEREZANI..

Leave A Reply