The House of Favourite Newspapers

Chivaviro Rasmi Ni Mwananchi… Yanga Yawazidi Ujanja Kaizer Chief Kutambulishwa

0
Ranga Chichaviro

DEAL Done! Rasmi sasa mshambuliaji wa Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini, Ranga Chichaviro amemalizana na uongozi wa Yanga huku akisubiria kutambulishwa pekee.

Yanga imepanga kuiboresha safu ya ushambuliaji kwa kumleta mshambuliaji huyo mwenye mabao sita sawa na Mkogomani wa timu hiyo, Fiston Mayele katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga hivi sasa inaongozwa na Mayele na Mzambia Kennedy Musonda ambao wameonekana kucheza kwa kuelewana tangu wacheze pamoja katika kikosi cha Nasreddine Nabi.

Championi Jumatano, lina taarifa kuwa Yanga inakaribia kuipata saini ya mshambuliaji huyo aliyefikia muafaka mzuri wa kusaini mkataba wa miaka miwili Jangwani.

Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Usajili ya Yanga, ameliambia gazeti hili kuwa ofa nzuri waliyoitoa kwa mshambuliaji huyo imetosha kumshawishi nyota kukubali kujiunga na timu hiyo, katika msimu ujao.

Kiongozi huyo alisema kuwa hivi sasa wapo uongozi wa ukiongozwa na Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said ambaye anasimamia dili wapo hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo baada ya yenyewe kuonyesha nia kubwa kuja Yanga.

Aliongoza kuwa Menejimenti ya Chivaviro imeichagua Yanga kutokana na ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu ujao, lengo likiwa ni kupata nafasi ya kuonekana kimataifa.

“Ni kweli uongozi wa Yanga tunaendelea na mazungumzo ya kukamilisha uhamisho wa Chivaviro, na uzuri kuwa Menejimenti ya mchezaji inatupa kipaumbele sisi kutokana na uhakika wa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

“Tayari ofa nono mezani kwa uongozi wa mchezaji, licha ya wenyewe kukiri kupokea ofa kadhaa katika baadhi ya klabu kubwa ikiwemo Kaizer Chief ambayo ina nafasi ndogo ya kumchukua.

“Ofa yetu ni nzuri zaidi aliyopeleka Rais Hersi Said, furaha kwa ranga kuja Tanzania hivyo dili hilo muda wowote litakamilishwa,” alisema kiongozi huyo.

Hersi juzi alithibitisha kusajili mmoja wa washambuliaji wakubwa Afrika Kusini “Tupo katika mazungumzo mazuri na mmoja wa washambuliaji wakubwa Afrika.

“Tupo katika mazungumzo mazuri, na muda wowote tunatarajia kukamilisha usajili wake ambao utakuwa gumzo, kikubwa tunataka kuwa mchezaji kutoka Afrika Kusini atakayeitangaza vema Yanga, kama ilivyokuwa kwa Mayele nyumbani kwao DR Congo.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

UTATA! KIFO CHA MC JOEL, KUHUSISHWA na DAWA? BABA AFUNGUKA UKWELI na SABABU, AWASHAURI VIJANA…

Leave A Reply