The House of Favourite Newspapers

CHRIS BROWN ATARAJIWA KUITWA BABA TENA

BAADA ya kuwa na mtoto mmoja wa kike, Loyalty, staa wa Muziki wa R&B, Chris Brown anatarajiwa kuitwa baba tena baada ya mpenzi wake, Ammika Harris kunasa ujauzito.

 

Wawili hao wameanza kutoka kimapenzi miaka miwili sasa ambapo uhusiano wao walikuwa wakifanya kwa siri.

Juzikati, Ammika aliachia picha mitandaoni akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na ndipo Chris aliingia na kukomenti; ‘My BM.’ Akimaanisa Baby Mama wake (mama wa mtoto).

 

Baada ya muda mfupi tena, Ammika alitupia picha zikimuonesha kitumbo kikianza kuchomoza jambo lililoamsha shangwe kwa mashabiki wa Chris.

LOS ANGELES, Marekani

Comments are closed.