Coldwell Banker Real Estate Yavutiwa na Soko la Mali Isiyohamishika
IKIWA na makadirio ya thamani ya dola za Marekani bilioni 1.5 kufikia mwaka 2019 ikilinganishwa na dola bilioni 1.2 mwaka 2015 na kuchangia asilimia 3.1 katika pato halisi la Taifa, sekta ya mali isiyohamishika ya Tanzania inaendelea kukua kwa kasi.
Kwa mujibu wa takwimu za Statista, soko la mali isiyohamishika nchini linatarajiwa kufikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 696.60 ifikapo mwisho wa mwaka (2024). Soko pia linakadiriwa kuongezeka kwa mahitaji ya mali za kifahari za ufukweni kwa sababu ya ukanda wake wa pwani mzuri na kukua kwa sekta ya utalii.
Ni muhimu pia kutambua kwamba kuna wimbi la uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika sekta ya majengo ya Tanzania ambao umesaidia kuongeza mitaji na utaalamu wa ziada, na hivyo kuchochea ukuaji na ubunifu ndani ya sekta hiyo.
Bila kuachwa nyuma na kwa kuvutiwa na atakwimu hizo, kampuni ya Coldwell Banker Real Estate LLC, imezindua biashara mpya kuu, Coldwell Banker Tanzania na Zanzibar Real Estate, ili kupanua mtandao wa chapa yake ya kimataifa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo (Mkurugenzi Mtendaji), Gina Washington, alisema wakati wa uzinduzi kuwa wanakusudia kuleta utaalamu wa kimataifa wa mali isiyohamishika wa chapa hiyo katika moja ya soko linakuwa la mali isiyohamishika la Afrika Mashariki.
“Pamoja na ukuaji wa haraka wa miji na ukuaji wa uchumi unaochochea mahitaji ya huduma za ubora wa juu wa majengo, biashara hii kuu iko katika nafasi nzuri ya kuwapa wateja wa ndani na nje ya nchi mwongozo na usaidizi usio na kifani katika kuvinjari mandhari ya Tanzania na Zanzibar inayostawi,” alisema.
Kampuni hiyo inayoendesha shughuli zake kutoka Mizizini mjini Zanzibar, imeanzisha kitengo chake cha kwanza cha makazi na biashara—Coldwell Banker Islemark Realty kwa udalali wa makazi na Coldwell Banker Commercial Blueridge kwa majengo ya kibiashara—ili kutoa huduma kwa wamiliki wa nyumba, wawekezaji na wafanyabiashara katika kisiwa hicho.
“Tuna mipango ya kufika katika maeneo mengine mengi zaidi kote nchini, na kuleta urithi wa karne za uadilifu na ubora kwa Afrika Mashariki, kukuza uhusiano wa kuaminika na kutoa huduma za hali ya juu za mali isiyohamishika iliyoundwa kukidhi mahitaji anuwai ya soko linalobadilika,” alisema.
Alibainisha kuwa kampuni imejikita katika kuleta maendeleo endelevu na ujenzi unaozingatia utunzaji wa mazingira, kuhakikisha thamani ya muda mrefu kwa wateja na jamii.
“Uwepo wetu hapa unaonyesha uwezo wa kuendelera kukua kwa soko la Tanzania na Zanzibar. Kwa uadilifu na kutumia ubunifu, tuko hapa kujenga mahusiano mazuri na jamii zinazotuzunguuka na kusaidia ukuaji chanya katika sekta ya mali isiyohamishika,” alibainisha.
Wakati mipango ya serikali Zanzibar ikiendelea kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje na sekta ya utalii kushamiri, kuna mahitaji makubwa ya miradi ya rejareja, ukarimu na makazi.
Chapa hii inatoa huduma za kina zilizoundwa kusaidia mahitaji haya, ikijumuisha mikakati ya uwekezaji, ukuzaji wa mradi na uwakilishi wa wapangaji.
Zaidi ya hayo, huduma za makazi za chapa kupitia mpango wa Coldwell Banker Global Luxury zitasaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya makazi ya hali ya juu, ukodishaji wa kifahari na fursa za uwekezaji wa makazi.
“Sekta ya mali isiyohamishika nchini Tanzania na Zanzibar inakabiliwa na ukuaji wa ajabu, na nina imani kuwa huu ni wakati muafaka kwetu kuleta utaalam maarufu wa chapa yetu katika eneo hili. Pamoja na huduma za makazi na biashara, mtandao wetu unaoaminika na utaalam usio na kifani utabadilisha jinsi sekta ya mali isiyohamishika inavyofanya shughuli zake,” alisema.
Jason Waugh, Rais wa Coldwell Banker Affiliates, alisema katika taarifa yake kwamba wanafurahi kujiunga na soko ambalo linatoa fursa nzuri na aliapa kutoa huduma ya kipekee na utaalam ambao chapa hiyo inajulikana ulimwenguni kote.
Tangu 1906, chapa hii imejijengea sifa ya kimataifa kama kiongozi anayeaminika katika sekta ya mali isiyohamishika, ikiwa na mtandao wa ofisi zaidi ya 3,000 katika karibu nchi 50. Chapa hii, inayojulikana kwa kulenga mteja, hutoa masuluhisho ya kiubunifu na ya kiteknolojia huku kwa wa uaminifu, kujitolea na utaalamu.
Takwimu zinaonyesha kuwa mahitaji ya majengo ya makazi nchini Tanzania yanatawala soko na makadirio ya soko la kiasi cha dola za Marekani bilioni 637.40 kwa mwaka 2024.
Data zinaonyesha eneo hilo linatarajiwa kukua kwa kiwango cha ukuaji wa kila mwaka cha asilimia 6.75 (CAGR 2024-2029), na kusababisha soko la dola bilioni 965.80 kufikia 2029.
Ikilinganishwa kimataifa, inafaa kufahamu kuwa Marekani inatarajiwa kutoa thamani ya juu zaidi katika soko la mali isiyohamishika, ikiwa na makadirio ya thamani ya dola za Marekani trilioni 132.0 mwaka 2024.
Ingawa takwimu zinaweza kuonekana kuwa za kawaida kwa kulinganisha, mwelekeo huo unaonyesha matumaini ya ukuaji na fursa za uwekezaji ndani ya mandhari ya mali isiyohamishika ya nchi kutokana na kupanuka kwa uchumi wa taifa unaochochewa na sera thabiti za uchumi na uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu na miradi ya maendeleo.
Wataalamu wanadokeza kuwa ukuaji wa uchumi umesababisha ongezeko la viwango vya mapato vinavyoweza kutumika, na hivyo kusababisha mahitaji ya fursa za uwekezaji wa nyumba na mali isiyohamishika. Wataalam pia wamehusisha ukuaji wa soko la mali isiyohamishika na ukuaji wa haraka wa miji na ongezzeko la idadi ya watu nchini.
Ukuaji wa uchumi umeshuhudia idadi kubwa ya watu wa vijijini wakihama kutoka vijijini kwenda mijini kutafuta ajira, elimu, na kuboresha hali ya maisha, ambayo husababisha kuongezeka kwa ukuaji wa miji na hitaji la makazi ya hali ya juu.
Mambo mengine yanayohusishwa na ukuaji huo ni sera zilizoboreshwa kama vile vivutio vya kodi kwa wakandarasi wa mali isiyohamishika, michakato ya udhibiti iliyoratibiwa, na ubia kati ya sekta ya umma na ya kibinafsi ambayo imewezesha ujenzi wa majengo ya makazi na biashara na kuchochea uwekezaji katika soko.
Annabelle Maimu, wakala wa mali isiyohamishika, alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya soko, wafanyabiashara wanabadilisha mikakati yao ili kukidhi mahitaji na matakwa ya walaji, kutoka kwa miradi ya nyumba za bei nafuu inayolenga sehemu za kipato cha kati na cha chini hadi maendeleo ya anasa yanayohusiana na thamani ya juu.
“Soko linashuhudia kuongezeka kwa chaguzi za makazi na biashara zinazoundwa kulingana na idadi ya watu,” aliongeza.
Nambari hazidanganyi kamwe, sekta ina uwezo mkubwa wa kuchangia maendeleo ya uchumi na ustawi wa taifa, na labda hakuwezi kuwa na wakati mwafaka zaidi kwa mwekezaji mpya.