DAKTARI ATOBOA SIRI NZITO WATU KUTAFUNA, KUMEZA VYUPA! (Video)
MAKUBWA! Daktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, Dk Godfrey Chale ameeleza kwa kina juu ya kitendo cha binadamu wa kawaida kutafuna na kumeza vipande vya chupa, wembe na vitu vingine vyenye ncha kali bila kudhurika, ikiwa ni pamoja kuanika kwa uwazi madhara ya jambo hilo, teremsha macho hapa chini.
Siku kadhaa zilizopita, kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Amosi Mawembe alitinga katika Studio za Global TV Online ambapo alionesha maajabu ya kuvunja chupa ya soda kisha kuvitafuna vipande vyake kabla ya kumiveza huku akisindikizia na maji.
SOMA: Park Ji-Sung Nitabaki Manchester Milele
Tukio hilo liliwaacha hoi wengi na kubaki na maswali juu ya nini hutokea hadi binadamu akaweza kufanya kitendo hicho cha ajabu, ilihali ikitokea kwa bahati mbaya mtu akameza kitu chenye ncha kali, huweza hata kumgharimu uhai wake.
Katika mahojiano hayo, Amosi alisema…h “Nimeanza kufanya hivyo tangu nikiwa mdogo na kamwe sijawahi kupata madhara yoyote na ni kazi ambayo ninaitegemea katika kujipatia kipato kama njia ya mazingaombwe.” Huku akishindwa kuweka wazi kwa undani juu ya nini hutokea kwa mhusika kufanya jambo hilo.
Ili kujiridhisha kwa maelezo ya kitaalam, mwandishi wetu alimtafuta Dk Chale kwa lengo la ufafanuzi ambapo alifika kwenye Studio za Global TV Online na kutoa ufafanuzi uliotoa mwanga juu ya madhara yake.
SOMA: Pendo Aibuka, Ataja Sababu Za Kuchukia Mapenzi!
“Ile ni tabia, kwamba ule mfumo wa chakula kuanzia mdomoni hadi tumboni, unakuwa ume-adopt mazingira ya kupokea vitu vigumu au vyenye ncha kali, kuna kitu kinaitwa mucous yaani ule ute mzito, mtu yeyote akiweka kitu chochote mdomoni kiwe laini au kigumu, ni lazima kinywa kitatoa ute mzito wa kukilainisha chakula hicho na kukisindikiza hadi mahali husika ambako ni tumboni.
“Sasa kiwango cha uzito wa ute huo au mucous kama nilivyosema kinategemeana na aina ya kitu kilichoingia mdomoni yaani kama ni kigumu ina maana ute unakuwa mzito zaidi na kama ni laini ute unakuwa wa kawaida, ndiyo maana ukiangalia kwa umakini mtu anayetafuna vipande vya chupa au wembe huwa anacheza na ncha ili ahakikishe zinakuwa zimeelekea wima kwa ndani na si kulala kwa upana.
“Ule ute huzuia ncha za vipande hivyo kuchoma moja kwa moja kwenye nyama laini za kinywa na hata utumbo, sasa hali hiyo ya ute mzito huwa inajijenga na kuzoea kutoka kwa wingi kama mhusika alianza tabia hiyo tangu mtoto au zamani, yaani mfumo huzoea na ndiyo maana wale wenzetu wenye matatizo ya akili wengine mnaita vichaa wanashinda jalalani wakila vipande vya miti na vyupa kama hivyo na hawadhuriki, lakini sasa inaweza ikatokea akakosea kuziweka sawa ncha za vyupa au siku hiyo akawa anaumwa hivyo kiwango cha ute mzito kinapungua, ni lazima atachanwa sana kinywani na damu nyingi zitamtoka na atachomwa kwenye utumbo wa chakula na asipofanyiwa upasuaji wa haraka uhai wake ni lazima uondoke na wakati mwingine kuchanwa vibaya sana kwenye sehemu za kutolea haja kubwa na mhusika hujisaidia damu nyingi, sishauri kabisa tabia hiyo na ni mbaya mno, hivyo haipaswi kuigwa,” alisema Dkt. Chale.
STORI: BRIGHTON MASALU, AMANI