DK CHENI AKIRI KUIPA KISOGO SANAA

 Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’

MKONGWE kwenye sanaa ya filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’ amefunguka kuwa, kwa sasa ameamua kuiweka pembeni sanaa na kujikita zaidi kwenye shughuli zake za U-mc. 

 

Dk Cheni amesema, kutokana na hali ya soko la sanaa ilivyo ameamua kujikita katika shughuli zake za sherehe kwa maana ya kupiga muziki, MC na kupiga picha kwani kwake ameona zinamuingizia kipato tofauti na uigizaji.

 

“Acha niusome kwanza mchezo kwa upande huu, sijaitupa sanaa moja kwa moja ipo siku mashabiki wanaweza kuniona kwenye gemu kama kawaida soko litakapokaa vizuri,” alisema Dk Cheni ambaye ni miongoni mwa wasanii waliokulia kwenye maadili ya vikundi vya sanaa vya mwanzoni mwanzoni vilivyoanza kuonesha maigizo yao kupitia televisheni.


Loading...

Toa comment