The House of Favourite Newspapers

DSTV Yamtambulisha Salama Jabir, Kutangaza Kiswahili AFCON 2019

Mtangazaji mpya wa Super Spoti kwa michuano ya Afcon 2019, Salama Jabir akifanya mahojiano na kituo cha Radio cha +255 Global Radio leo, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

 

MultiChoice Tanzania imetambulisha kampeni yao mpya ya Tupogo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019  ‘AFCON’  nchini Misri kupitia + 255 Global Radio iliyopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Juni 21 ambapo Tanzania ipo kundi C ikiwa na timu nyingine ambazo ni Kenya, Senegal na Algeria.

Afisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa akiongea jambo wakati wa mahojiano hayo na +255 Global Radio.

Ofisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa kupitia +255 Global Radio  alisema wateja wanaotumia king’amuzi cha DSTV  watawapa nafasi ya kuangalia mechi hizo kwa lugha ya Kiswahili, huku kivutio akiwa mtangazaji mpya wa michezo Salama Jabir ambaye atatangaza mpira kwa mara ya kwanza kwa Lugha ya Kiswahili.

Mtangazaji wa vipindi vya Michezo, Ibrahim Masoud ‘Maestro’.

Watangazaji wengine watakaotangaza michuano hiyo kupitia Super Sport  ni pamoja na Ibrahim Masoud ‘Maestro’ , Maulid kitenge na Edo Kumwembe, amewaomba watanzania ambao hawatumii DSTV kujipatia king’amuzi ambacho kimeshaunganishwa na kifurushi cha Compact kwa 99,000/- ambacho kifurushi hicho kitakuonyesha  mechi zote za michuano hiyo ya AFCON. Kwa wakazi wa Dar, piga namba hii 0659070707 utaletewa ulipo pamoja na huduma ya ufundi pia amesema kwa watazamaji wa kawaida wataweza kutazama mechi hizo 52 kupitia kifurushi cha DSTV bomba kwa lugha ya Kiswahili.

Pia mchambuzi mkongwe nchini, Masoud Maestro alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuja kuwapa watanzania burudani ya uchambuzi mzuri pamoja na kufurahia Lugha adhimu ya Kiswahili.

PICHA: SWEETBERT LUKONGE, GPL

Comments are closed.