The House of Favourite Newspapers

ESHA BUHETI FULL SHANGWE KWA KUJIFUNGUA SALAMA

0
ESHA BUHETI
Esha Buheti

Baada ya msanii Linah, mwanamitindo Faiza Ally na Hamisa Mobetto kujifungua salama, sasa ni zamu ya diva kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Esha Buheti ambaye naye amejifungua leo.

Esha amejifungua mtoto wa kike leo, katika hospitali ya Sali International iliyopo ushuani Masaki. Na kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha taarifa hizo kwa kupost picha ya kichanga chake na kuandika maneno yafuatayo.

Alhamdullilah ni mtoto wa kike, asante Mungu kwa zawadi hii, asanteni wote kwa dua zenu mimi na mtoto tupo salama.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply