Uchaguzi huo umetanguliwa na Mkutano Mkuu wa TFF ambao umezinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ukiwa na ajenda 14 zikiwemo kutambulisha wajumbe, kupitisha wagombea na ajenda ya uchaguzi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, Dkt. Mwakyembe amewasisitiza wajumbe wanaoshiriki uchaguzi huo kuzingatia kanuni za utawala bora ili kuleta tija katika maendeleo ya soka hapa nchini.
Waliohudhuria uchaguzi huo ni pamoja na Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi, pia wajumbe wa CAF na Fifa ambao wameona mchakato wa uchaguzi utachelewa kulingana na jinsi mipangilio yao ilivyo, hivyo na wao wameshauri mkutano ufanyike haraka ili waanze shughuli ya uchaguzi mara moja.
Timu ya Global TV ipo Dodoma, itakuhabarisha hatua kwa hatua kuhusu uchaguzi huo.
PICHA: MUSA MATEJA
VIDEO NA MOHAMMED ZENGWA | GLOBAL TV | DODOMA
[…] Mwakyembe Ataja Vigezo kwa Uongozi Unaotakiwa TFF […]