The House of Favourite Newspapers

Global FC Yailambisha Mchanga Sinza Veterani

Kikosi cha Global FC.

Nahodha wa timu maarufu ya soka Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Sinza Boys Veterani, Ali Ngoti amesema licha ya kufungwa 4-3 na Timu ya Global FC, wanaamini mechi inayofuata watalipa kisasi kwani hawadhani wao ni wa kufungwa kirahisi.

Kikosi cha Sinza Veterani.

Akizungumza na mtandao huu, Ngoti alisema timu yao ilikuwa imejipanga kwa ushindi mnono lakini makosa madogo waliyofanya ndiyo yaliyosababisha washindwe kung’ara.

Beki wa Global FC, Omary Mdose akimzuia mchezaji wa Sinza Veterani.

“Global FC ni timu nzuri sana, wachezaji wake wanajua kutandaza soka lakini sisi licha ya ukongwe wetu, hatuamini kwamba ni wa kufungwa kirahisirahisi.

…..krosiiiiii

“Tunakwenda mafichoni, tukiibuka tunataka mechi tena na naamini tutalipa kisasi, sisi siyo wa mchezomchezo, waliowahi kucheza na sisi wanajua mziki wetu, kwa hiyo Global wajipange kweli, safari nyingine tukikutana tunawaaibisha,” alisema Ngoti.

….mbwembwe uwanjani

Naye kepteni wa Global FC, Wilbert Moland alisema: “Kipigo cha bao 4-3 walichokipata Sinza Veterani kiliwastahili, kama wanaona tulibahatisha, wajipange upya, nakuhakikishia tukikutana tena tunawapiga hamsa.”

Mashabiki wa Global FC wakishangilia.

Sinza Boys Veretani na Global FC inayodhaminiwa na Kampuni ya Ashishi Cinematographer walikipiga kwenye uwanja wa Mashujaa uliopo Sinza Kumekucha na wanatarajiwa kurudiana hivi karibuni.

Mchezaji wa Sinza Veterani akiwatoka wachezaji wa Globa FC.

Aidha, Global FC ambayo mwaka huu imefanya usajili wa kutisha iko kambini ikijiandaa na mechi na  timu kubwa Bongo. Ni timu gani hiyo? Kaa mkao wa kusikilizia. Kumbuka michezo ni afya!

Imeandikwa na Amran Kaima.SAID ALLY, Dar es Salaam

Comments are closed.