The House of Favourite Newspapers

Godbless Lema: Yeriko Nyerere Amekamatwa au Ametekwa?

0
Yeriko Nyerere

KUFUATIA kada wa CHADEMA na mdau wa mitandao ya kijamii, Yericko Nyerere kukamatwa na watu wanaodaiwa kuwa Polisi akiwa nyumbani kwake, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema ameuliza swali je, Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa?

 Lema ameuliza swali hilo katika ukurasa  wake wa Twitter leo na kuongeza: “Msiogope. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea.

 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
Ikumbukwe hii ni Mara ya pili kukamatwa kwake, baada ya kesi yake iliyodumu Kwa miaka miwili tangu kipindi cha uchaguzi ambapo alishinda na kuachiwa huru mapema April 2017.
Yeriko anayefahamika kuwa ni kada wa Chadema, amekamatwa leo saa tisa alfajiri na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi akiwa nyumbani kwake, Kigamboni, Mbutu.
 
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Yeriko.
===========================

BreakingNews: IGP Sirro Aanza na Mauaji Rufiji, Kibiti na Ikwiriri Mkuranga, Asema Ubaya Ubaya Tu!

Leave A Reply