Griezmann aiacha gizani Atletico

RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amedai hadi sasa hafahamu timu ambayo staa wao Antoine Griezmann anataka kujiunga nayo.

 

Kauli ya Cerezo inazua wasiwasi kuhusiana na mustakabali wa straika Griezmann.

Hali hiyo inaashiria kuwa Barcelona hawajaanza mazungumzo yoyote na Atletico juu ya kumchukua Griezmann. Wakati msimu huu wa 2018/19 unakaribia kumalizika, Griezmann aliwaeleza viongozi wa Barcelona kuwa anataka kuhama.

 

Watu wengi walikuwa wanaamini kuwa Griezmann kuwa anakwenda zake Barcelona.NBarcelona ilitaka kumchukua mwanzoni mwa msimu huu lakini Griezmann alibadili mawazo na kuongeza mkataba wa kuchezea Atletico hadi waka 2023.

 

“Griezmann amekuwa nasi kwa miaka mitano ila kusema ukweli sijafahamu hadi sasa ana mpango wa kujiunga na timu gani,” aliongeza Cerezo

Loading...

Toa comment