×

Harmonize: Usikubali Mtu Akukatishe Tamaa, Pambania Ndoto Zako

Harmonize maarufu kama Konde Boy “Teacher”

HARMONIZE au Teacher Konde; ni staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania ambaye anasema kuwa wakati anahaso kutoka kimuziki alikatishwa tamaa mno hasa alipokuwa anajitoa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ya mtu mzima Diamond Platnumz.

 

Harmonize au Bakhresa anasema; “Usiruhusu mtu akwambie kwamba huwezi, amka na uzifuate ndoto zako. Nitazame mimi, nilipoanza safari yangu ya muziki, kila mmoja alikuwa akinikejeli kwamba nitafanya nini kwenye kiwanda cha muziki? Nikawaambia nitafanya nitakachoweza kufanya.

Harmonize au Bakhreza amesema vijana wasikubali kuvunjwa moyo kwenye kupambania ndoto zao

“Na nilipotoka kwenye lebo yangu ya zamani (WCB) kila mmoja alikuwa akisema nimeisha, nitakufa Kimuziki. Nitazame sasa hivi, mimi ni mshindi. Na Konde Gang ni lebo namba moja Tanzania kwa sasa, Afrika Mashariki na tunaitafuta Afrika sasa hivi.”

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment