Hasheem Thabeet Aitwa Timu ya Taifa

UONGOZI wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), jana ulitangaza kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa mchezo huo kitakachoiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kanda ya Tano (Zone 5), Juni 25, mwaka huu nchini Uganda.

 

Rais wa TBF, Phares Magesa, alisema jumla ya wachezaji 63 wameitwa kuunda timu ya taifa ambapo wanaume ni 34 akiwemo Hasheem Thabeet na wanawake 29 ambapo mazoezi yataanza Mei 29, mwaka huu.

 

Magesa aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini, pamoja na kusafiri kwenda kwenye mashindano hayo kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya All African Games kuelekea Olimpiki 2020.

 

Kwa upande wake, kocha mkuu wa timu ya wanaume, Ashraf Haroon, alisema kupitia mazoezi hayo, wataanza na wachezaji ambao wapo hapa nyumbani huku wale wanaocheza ligi za nje ya Tanzania wataendelea kufanyiwa utaratibu ili watue nchini kujumuika na wenzao.

 

“Tunakabiliwa na michuano ya Zone 5 ambapo kwa upande wa Tanzania tutawakilishwa na timu ya wanaume na wanawake, kwa upande wa wachezaji tumeshaorodhesha majina yao kwa kuanza kambi na mazoezi mwishoni mwa mwezi huu


Loading...

Toa comment