The House of Favourite Newspapers
gunners X

Hazard: Asanteni Chelsea, kwaherini

EDEN Hazard, juzi usiku alifunga mabao mawili na kuiwezesha timu yake ya Chelsea kubeba ubingwa wa Europa League dhidi ya Arsenal, lakini baada ya hapo akatoa kauli ya kuaga.

 

Staa huyo ambaye amekuwa akihusishwa kuelekeka Real Madrid, alionyesha uwezo wajuu na kuchangia ushindi wa mabao 4-1, baada ya hapo akasema huu ni muda wa kutafuta changamoto mpya kwake.

 

Kauli hiyo ni wazi kuwa amewaaga Chelsea na sasa yuko tayari kwenda Madrid ambako anadaiwa kuwa atatua kwa ada ya pauni milioni 115.

 

Baada ya mchezo huo wa juzi, alihojiwa kuhusu hatima yake akiwa uwanjani na kusema: “Sijajua bado lakini najua itaamuliwa ndani ya siku chache zijazo. “Lengo langu la leo kwanza ilikuwa ni kubeba ubingwa, hilo limetimia, nimeshafanya maamuzi yangu tayari kama nilivyosema wiki chache zilizopita.

 

“Hilo sasa litategemea na maamuzi ya klabu zote, nasubiri maamuzi yao kama ambavyo mashabiki wanasubiri. Nafikiri huu ni mchezo wa kuwaaga, lakini katika soka huwezi kujua, lolote linaweza kutokea,” alisema na kuongeza: “Ndoto yangu ilikuwa ni kucheza Premier League. Nimefanya hivyo kwa miaka saba katika moja ya klabu kubwa duniani, sasa nahitaji changamoto mpya.”

MO AWARDS: KOTEI Ashinda TUZO ya KIUNGO Bora, Afunguka Haya!

Comments are closed.