The House of Favourite Newspapers

Hospitali ya Afrika Kusini Yachunguzwa kwa Kuwaweka Watoto Wachanga Kwenye Boksi

0

Mamlaka ya Afrika Kusini inachunguza tukio ambapo watoto wachanga waliwekwa kwenye masanduku ya kadibodi, badala vitanda maalum vya watoto wachanga katika jimbo la Kaskazini Magharibi.

Tukio hilo katika sehemu ya watoto wachanga katika Hospitali ya Mkoa wa Mahikeng lilidhihirika siku ya Jumamosi baada ya chapisho la Facebook kuonyesha watoto wakiwa wamevikwa blanketi za hospitali za zambarau na mirija ya puani na kuwekwa kwenye masanduku ya kahawia, vyombo vya habari vya ndani vilisema.

Mkuu wa afya Kaskazini Magharibi Madoda Sambatha alisema wanachunguza suala hilo ili kubaini ni muda gani watoto hao walikaa kwenye masanduku hayo.

Sambatha aliomba msamaha na akaomba utulivu wakati suala hilo likichunguzwa.

Alisema, kwa dharura, utaratibu ulifanywa ili vitanda vya ziada vipelekwe hospitalini.

Meneja wa hospitali hiyo ameripotiwa kusimamishwa kazi.

Waziri wa Afya Joe Phaahla mnamo Jumatatu alielezea tukio hilo kama usimamizi duni wa wale wanaosimamia kituo hicho.

MPINA KUDAIWA KUPORA ARDHI ya WANANCHI/ POLISI GUMZO BUNGENI/ PACHA WAFA WAKIOGELEA |FRONT

Leave A Reply