The House of Favourite Newspapers

Injinia Hersi: Wachezaji Wametuapia Kuifunga Simba Kesho Kutwa Jumapili

0
Rais wa Klabu ya Yanga, Eng Hersi Said.

WACHEZAJI wa Yanga kwa pamoja wamewaahidi viongozi wa timu hiyo, kupambana kwa dakika 90 ili kuhakikisha wanarejesha furaha ya mashabiki, watakapovaana na Simba keshokutwa Jumapili.

 

Dabi hiyo inatarajiwa kuzikutanisha Yanga na Simba katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Timu hiyo, juzi Jumatatu ilirejea kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mara baada ya kutoka kutolewa na Al Hilal katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzana Championi Ijumaa, Hersi alisema kuwa mara baada ya timu hiyo kuingia kambini uongozi ulifanya kikao na wachezaji ambao walionekana kusikitishwa na kuumizwa na matokeo dhidi ya Al Hilal ambayo yamewakera mashabiki wa Yanga.

 

Hersi alisema kuwa katika kuelekea dabi hiyo, wachezaji wameahidi kupambana kufa au kupona ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri yatakayorudisha imani ya Wanayanga.

 

Aliongeza kuwa mara baada ya kikao hicho, wachezaji hao walihimizana kila mmoja kutimiza majukumu yake ya uwanjani pale atakapopata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

 

“Wachezaji wanajutia makosa yao waliyoyafanya ambayo yamesababisha kushindwa kufikia malengo ya kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

 

“Hivyo wameahidi kurejesha imani ya mashabiki wa Yanga kwa kushinda katika dabi hii, ni baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kila mmoja ameahidi kuipambania timu katika mchezo huo.

 

“Tunafahamu haitakuwa rahisi, lakini wachezaji wenyewe upande wao wametoa ahadi hiyo kubwa ambayo ikifanikiwa, basi ninaamini mashabiki watarudisha Imani kwa timu yao,” alisema Hersi.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

KISA YANGA MODEWJI AMTANGAZIA MINOTI MGUNDA, HERSI WACHEZAJI WAMETUAPIA KUIFUNGA SIMBA..

Leave A Reply