ISHU YA FREEMASON… YATIKISA UPYA WASAFI!

KUMEPITA ukimya wa muda mrefu hazijasikika zile habari za msisimko zinazoihusu jamii ya siri duniani inayodaiwa kumuabudu shetani na kuhusishwa na utajiri wa ghafla ambao si wa kawaida ya Freemason hapa nchini, Amani linaibuka nayo.

 

Madai mapya juu ya Freemason inayodaiwa kuhusika na makafara ya damu, yanaigusa familia kubwa ya mastaa wa muziki wa Bongo Fleva chini ya mwavuli wa Wasafi Classic Baby (WCB).

 

Wasafi inajengwa na mastaa wakali walioishika Bongo Fleva wakiongozwa na bosi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’. Wengine ni Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Konde Boy’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ au ‘Chuma’, Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ au ‘Khan’, Abdul Idd ‘Lava Lava’ na first lady wao, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.

WASAFI NA FREEMASON

Madai dhidi ya Lebo ya Wasafi kuhusishwa na Freemason yameibuka upya baada ya jamaa hao kuiteka Bongo kwa shoo kubwa kila kona ya nchi katika Sikukuu ya Idd hivi karibuni. Kufuatia mafanikio hayo, madai ya mtandaoni ni kwamba, jamaa hao wamepata mafanikio ya harakaharaka kwa msaada wa Freemason.

 

Inadaiwa kuwa, mbali na kufunika kwa shoo hizo na kupata utajiri wa ghafla katika siku za hivi karibuni, lakini pia Freemason wanahusika na kung’arisha nyota zao na kuwafanya kukubalika ile mbaya ndani na nje ya Bongo.

 

Katika shoo zao za Idd, Diamond alitikisa Miji ya Kahama na Geita, Harmonize na Queen Darleen wakaujaza Uwanja wa Nangwanda- Sijaona mjini Mtwara na Rayvanny akateka Jiji la Dar katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem. Kwa upande wake Mbosso alifunga mitaa ya jijini Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani huku Lava Lava akifanya kweli mkoani Kigoma kwenye Ufukwe wa Aqua.

TURUDI KWENYE MADAI

Kwa mujibu wa madai ya mitandaoni, wasanii hao wamekuwa wakivaa mavazi, cheni na pete zenye nembo za Freemason kama sehemu ya masharti ya kuwa wanachama wake. “Kinachowaponza ni mavazi yao, cheni na pete zenye nembo za Freemason ambazo huwafanya kung’ara popote wanapokuwa.

 

“Ukiacha mavazi kuna ishara mbalimbali ambazo zinaaminika hutumiwa na Freemason. “Hata salamu zao wanazotumia mara nyingi ni zile zinazotengeneza nembo ya Freemason ya “V” na bikari hasa kwenye kukunja vidole. Hii nayo inawaponza,” kilisema chanzo hicho na kuongeza; “Picha inayotumika kuwahusisha na Freemason ni ile ambayo wanaonekana wote wakiwa kwenye mavazi meusi na pete na cheni zenye alama ya kama msalaba inayoitwa Cross and Crown.

 

“Hii Cross and Crown ni nembo ya Freemason inayomaanisha ushindi dhidi ya kifo. “Kwa kawaida cheni hizo pia huwa na maandishi yanayosomeka ‘In Hoc Signo Vinces’ kwa Kilatini na kwa Kiingereza husomeka ‘By this sign thou shalt conquer’ yakimaanisha kwa alama hiyo watashinda,” kilisema chanzo cha karibu cha mastaa hao wa Wasafi.

MENEJA AFUNGUKA

Mmoja wa mameneja wa Wasafi aliyezungumza na Gazeti la Amani juu ya ishu hiyo, Said Fela alianika ukweli wa anachokijua juu ya jambo hilo.

 

“Kwenye mafanikio ya wasanii wetu yanasemwa mengi, wengine wanasema tunaloga na wengine hayo mambo ya Freemason, lakini ukweli hakuna kitu kama hicho. “Siri ya mafanikio ya Wasafi ni kujituma kwa wasanii na uongozi makini hayo mengine hayana ukweli wowote,” alisema Fela.

 

DIAMOND NA FREEMASON

Ukiwaacha memba wengine wa Wasafi, lakini miaka kadhaa Diamond alihusishwa na Freemason ambapo aliwahi kufafanua suala hilo kupitia magazeti pendwa yanayoongoza kusomwa na wengi nchini Tanzania ya Global Publishers ambapo alisema; “Ni stori tu ambazo hata mimi nazisikia kama wewe (mwandishi), lakini sifahamu chochote juu ya mambo ya Freemason.”

 

FREEMASONI NI NINI?

Freemason ni jamii ya siri inayohusishwa na dini ya kishetani na watu wengi maarufu wanatajwa kuwa humo wakiwemo viongozi wa nchi mbalimbali na mastaa wengine kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye West na Celine Dion.


Loading...

Toa comment