×

Issa Gavu Amtaka Salim Abri ‘ASAS’Dairies Farm Kuweka Shamba Darasa la Mifugo Iringa

Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Gavu amefanya ziara katika shamba la Salim Abri maarufu (Asas) Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Iringa na kujionea namna ya ufugaji wa Kisasa katika Shamba hilo Dairies Farm Igingilanyi Mkoa wa Iringa.
Ndg. Gavu ameutaka uongozi wa Dairies Farm kuandaa eneo la Shamba darasa ambalo litakuwa sehemu ya kujifunzia kwa wafugaji wa ndani na nje ya nchi ili kupata elimu ya namna ya kufuga kisasa na wenye kuleta tija na faida katika Jamii.

Leave a Comment