The House of Favourite Newspapers

JPM ATANGAZA SIKU 4 ZA MAOMBOLEZO, WAHUSIKA WAKAMATWE

Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza Bendera ya Taifa kupepea nusu mlingoti kwa siku nne kuanzia leo Septemba 21 hadi Septemba 24, kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyotokea jana katika ziwa Victoria mkoani Mwanza na kuagiza wahusika wote wakamatwe na kuhojiwa na watakaokutwa na hatia wachukuliwe hatua.

 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea Mkoani Mwanza  mpaka sasa  jumla ya watu 131 wamepoteza maisha huku wengine 40 wakiokolewa .

 

Balozi John Kijazi ameongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kivuko hicho kilibeba abiria zaidi ya uwezo wake na kwamba kuanzia kesho bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kama ishara ya kuomboleza msiba.

 

BREAKING: RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA AJALI YA MV NYERERE

Comments are closed.