The House of Favourite Newspapers

JPM Awasili Kwenye Uzinduzi wa Barabara, Biharamulo

0
Rais John Magufuli.

 

Rais John Magufuli amewasili katika stendi ya Biharamulo mkoani Kagera ambapo unafanyika uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma- Biharamulo-Lusahunga.

Pamoja na uzinduzi Rais Magufuli pia atahutubia wananchi ambako umati mkubwa umehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 154.

Mwezi uliopita Rais  Magufuli aliweka jiwe la msingi kuashiria  ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.

Sambamba na hilo pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya Barabara za Nyerere na Mandela eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Leave A Reply