Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba, John Mnyika jana Desemba 29, 2019, alisimikwa kuwa Chifu wa Kabila la Wasukuma na kupewa jina la Maronja likiwa na maana ya MREKEBISHAJI.

Mnyika ambaye yupo mapumzikoni nyumbani kwao mkoani Mwanza, amepewa Uchifu na wanachama wa chama hicho mkoani humo ikiwa ni ishara ya ushindi katika kukiongoza chama hicho.
