The House of Favourite Newspapers

JPM AZINDUA KIWANDA CHA JWTZ, AMPA MAKONDA MAJI ANYWE PAPO HAPO – VIDEO

RAIS John Magufuli leo amezindua Kituo cha Uwekezaji cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia SUMA-JKT kilichopo eneo la Mgulani jijini Dar es Salaam ambacho kina Kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi, Shule ya Sekondari Jitegemee na Ukumbi wa Mikutano.

Katika uzinduzi huo, alisema atakuwa mdau mkubwa wa kununua maji ya Uhuru Peak yanayotengenezwa na kiwanda hicho akizisihi pia kwa taasisi na ofisi za serikali ikiwezekana zitumie maji hayo maofisini mwao badala ya kutumia maji mengine ili kuongeza uchumi na kusapoti viwanda vya JWTZ na vya serikali kwa jumla.

“Kuanzia leo mimi nitakuwa mdau mkubwa wa kutumia maji yenu ya Uhuru Peak, nitashangaa sana kukuta CDF, kiongozi yeyote wa Jeshi la Ulinzi au mkuu wa mkoa ananikaribisha ofisini kwake halafu nakuta kuna maji mengine tofauti na ya Uhuru Peak.

“Tulikuwa tumezoea kila nguo ya jeshi lazima tuagize kutoka nje, na unatumia dola, unawapa watu hao ajira, lakini leo nguo za jeshi letu tunatengeneza wenyewe hapahapa, tunaongeza ajira, hii inafaa sana,” alisema.

Aidha, Rais aliomba chupa ya maji hayo ya Uhuru Peak na kunywa papohapo, huku akiagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda naye apewe na anywe papohapo na kwamba Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi apewe, ili ayanywe wakati akifungua mfungo wa Ramadhan  jioni.

MSIKIE RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA

Comments are closed.