Kartra

Kabangu: Nawasubiria tu Simba

MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya DR Congo Kadima Kabangu amesema kuwa anawasubiri Simba wamalize michezo ya ligi kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam FA, ili aweze kufanya mipango ya kuja nchini kukamilisha mazungumzo ya usajili wake.

Kabangu ameweka wazi kufanya mazungumzo na kocha mkuu wa kikosi cha Simba, Didier Gomes.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kabangu alisema kuwa viongozi wa Simba walimwambia kwamba asubiri wamalize mashindano ambayo wanashiriki kwa sasa ikiwa ni pamoja na Kombe la Shirikisho pamoja na ligi ili waweze kufanya mazungumzo ya kukamilisha usajili.

 

“Tayari nimeshaongea na Simba kuhusu ishu ya usajili na kwa sasa nawasubiri tu wao wakamilishe michezo ya ligi pamoja na kombe la FA ili niweze kukamilisha usajili wangu ikiwa ni pamoja na kuja Tanzania.

 

Simba wao ndiyo wameniambia hivyo,kocha Gomes yeye amenithibitishia kuwa nipo katika mipango yake kwa ajili ya msimu ujao na mimi nipo tayari kujiunga na Simba na kilichobaki nawasubiri tu wao,”alisema mchezaji huyo.

STORI NA MARCO MZUMBE | GPL


Toa comment