Kagere Abeba Tuzo ya Tatu

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amechaguliwa na kamati ya tuzo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu kwa Mwezi Mei.

 

Kagere ametwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake wawili aliofi ka nao fainali ambao ni Bigirimana Blaise ambaye ni mshambulijai wa Alliance FC na Tariq Kiakala wa Biashara United.

 

Hii inakuwa tuzo yake ya tatu kutwaa msimu wa mwaka 2018/19 ndani ya TPL baada ya ile ya kwanza kuitwaa mwezi Agosti ya pili Februari na hii ya mwezi Mei kuwa ya tatu akimuacha mbali mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo mwenye tuzo mbili za TPL alizotwaa mwezi Novemba na Desemba, mwaka jana.

 

Kwa upande wa kocha bora wa mwezi, Etienne Ndayiragije wa KMC ametwaa tuzo hiyo akiwashinda makocha wenzake wawili ambao ni Patrick Aussems wa Simba na Malale Hamsini wa Alliance FC.

Loading...

Toa comment