Kajala Kisogo Maisha ya Starehe

Kajala Masanja

MWANAMAMA wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka kuwa, kwa sasa ameamua kuyapa kisogo maisha ya kuendekeza starehe hivyo mambo yanayoendelea kwenye ulimwengu wa starehe na burudani hana mpango nayo.

Akichonga na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Kajala alisema ameamua kuachana na mambo hayo kutokana na umri wake pia kuwa kwa sasa ana mtoto mkubwa ambaye anafuatilia kila kitu anachokifanya hivyo ameamua kutuliza akili kufanya mambo ya maana ambayo yatamuelimisha mwanaye Paula.


“Kuna umri unafika mtu unaachana na kila kitu na mambo ambayo hayaeleweki, nimeamua kutulia kwa sasa maana mwanangu Paula ameshakua, anaangalia matendo yangu kama mama yake kwa hiyo lazima nifanye mambo ya kumfundisha,” alisema Kajala.

LAVALAVA Amwaga MACHOZI Stejini AKIIMBA WASAFI FESTIVAL..

STORI NA IMELDA MTEMA


Loading...

Toa comment