The House of Favourite Newspapers

Masikini Kim Kardashian Hana Uwezo wa Kuzaa

1

MWANAMITINDO aliyejaa vituko kila kukicha Kim Kardashian, ambaye pia ni mke wa mwanamuziki wa Hip Hop Marekani Kanye West amepoteza uwezo wa kuzaa tena baada ya kupata tatizo la accreta ya plasenta, tatizo ambalo limepelekea madaktari kumzuia asibebe tena ujauzito kwani atahatarisha maisha yake.

Couple hiyo ambayo imebarikiwa watoto wawili wa kike na wa kiume Saint West  mwenye miezi 18,na North West mwenye miaka 4,lakini kwa sasa wametamani kuongeza mtoto wa tatu na kutokana na hali ya Kim imewabidi kuajiri mwanamke ambae  atapandikizwa mbegu zao ili abebe mimba ya mtoto wao wa tatu kwa gharama ya dola 45,000 (Zaidi ya milioni 80) kwa miezi 10 na nyongeza ya dola 5,000 (zaidi ya milioni 10) kama watapatikana watoto mapacha.

Wanawake wanaofanya kazi hii huko majuu huitwa surrogate mothers ambapo mkataba unaelekeza kuwa mwanamke huyo atakuwa chini ya uangalizi mkubwa haruhusiwi kuvuta sigara, kunywa pombe au kufanya kitu chochote ambacho kitamuathiri mtoto.

Na: ISRI MOHAMED

 

1 Comment
  1. […] ameibuka gumzo mitandaoni baada ya kukataa zawadi alizoletewa na Mwanamitindo maarufu nchini humo Kim Kardashian, kwa ajili ya watoto wake mapacha aliojifungua mwezi […]

Leave A Reply