Kisa Waarabu…Yanga Yashusha Mtaalam Mpya

ILI kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kabla ya kuwavaa Waarabu, timu ya Pyramids kutoka nchini Misri, uongozi wa Yanga umeongeza nguvu katika benchi la ufundi kwa kumleta daktari mwingine.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, wameongeza nguvu katika upande wa madaktari ili kupunguza majeruhi yasiyokuwa ya lazima.

 

“Tumeongeza nguvu upande wa madaktari ambapo kuna baadhi ya madaktari tumewaongeza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi dhidi ya Pyramids ili kupunguza majeruhi ambayo yatakuwa si ya lazima.

“Madaktari watakuwa karibu na kila mchezaji kwa kuwaangalia mmoja mmoja ili kuhakikisha wanajilinda tukiwa na lengo la kumsaidia kocha, Mwinyi Zahera aweze kuwa na kikosi kipana kitakachomsaidia.

 

“Wachezaji ambao walikuwa majeruhi wanaendelea kuimarika na wanapatiwa matibabu kwa ukaribu zaidi kuhakikisha wanakuwa fiti haraka,” alisema Mwakalebela ambaye amewahi kuwa kiongozi wa Mtibwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

STORI KHADIJA MNGWAI, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment