×

Rasmi Kotei Avunja Mkataba Kaizer Chiefs

KIUNGO mkabaji wa zamani wa Simba, James Kotei, amethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Kaizer Chiefs inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae kuwa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa usiku wa kuamkia leo.

 

Kotei tangu ajiunge na Kaizer Chiefs msimu huu, ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, hali iliyomfanya kuamua kuvunja mkataba.

 

“Ni kweli mimi na Kaizer Chiefs tumefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na sasa nipo huru kujiunga na timu yoyote. Nimepokea ofa mbili lakini bado tupo kwenye mazungumzo,” alisema Kotei.

STORI NA WILBERT MOLANDI

NUNUA GAZETI LA AMANI LEO JANUARI 16, 2020 kirahisi kabisa kupitia GlobalApp kwa Tsh 400/-bonyeza hapa 👇

GAZETI LA SpotiXtra => https://bit.ly/2TqcAMe

GAZETI LA AMANI=> https://bit.ly/2RnOpeO
AU
GAZETI LA AMANI=> https://bit.ly/2FQog35

Leave a Comment