Kocha Simba Anasa Faili la Red Arrows

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Mhispania Pablo Franco amefunguka kuwa amenasa mbinu zote ambazo wapinzani wake kwenye Kombe la Shirikisho kutoka Zambia, Red Arrows wanatumia.

 

Pablo alisema kwa zaidi ya wiki sasa amekuwa akitenga muda wake na kuzitazama mechi za Red Arrows na amebaini kuwa timu hiyo inacheza kwa kutumia sana nguvu na umoja wakati wote wa mchezo.

Simba na Red Arrows watashuka dimbani kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa kucheza mechi ya kuwania kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Pablo alisema: “Nimetumia muda mwingi sana kuwasoma Red Arrows na nimegundua kuwa ni aina ya timu ambayo mbinu yake kubwa ni kucheza kwa nguvu kwa dakika zote za mchezo.

 

“Hawana wachezaji bora zaidi ya Simba ila uimara wao upo kwenye kucheza kwa umoja na sisi tumegundua hilo na tulianza kulifanyia kazi haraka.”

STORI NA ISSA LIPONDA | CHAMPIONI JUMAMOSI

 VOA: OUR VOICES 344 – FEAST OR FAMINE? FOOD INSECURITY IN AFRICA….704
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment