×

Rais Yoweli Museveni Anawasili Nchini- (Picha +Video)

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameongoza mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Novemba, 2021 aliyewasili nchini kwa ajili ya ziara ya Kitaifa ya siku tatu hapa nchini.

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewasili nchini leo Novemba 27, 2021 kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu siku. Rais Museveni amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokewa na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan na kwa pamoja watafanya mazungumzo ya faragha na kufuatiwa na mazungumzo rasmi.

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, akikagua Gwaride la JWTZ mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Novemba, 2021 mara baada ya kuwasili nchini.

Leave a Comment