Kuwaona Balinya, Falcao Sh 50,000

UONGOZI wa Yanga umeweka hadharani viingilio vyake kuelekea mchezo wa dhidi ya Township Rollers ya Botswana wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kingilio cha juu kitakuwa ni Sh 50,000.

 

Katika mchezo huo ambao Yanga itakuwa na mastaa wapya wakiwemo Juma Balinga, David Molinga ‘Falco’, Patrick Sibomana na wengine kibao ambao wataitumikia klabu hiyo kwa mara ya kwanza, utapigwa saa 12 Jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

 

Kuelekea mchezo huo, ukiachana na kiingilio cha Sh 50,000 kwa VIP pia viingilio vingine ni Sh 15,000 kwa VIP B na C wakati mzunguko ikiwa ni Sh 5,000. Yanga kwa sasa ipo kambini visiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo huo wa Jumamosi na inatarajiwa kurejea jijini Dar muda wowote kuanzia sasa.


Loading...

Toa comment