The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kwagilwa Aagiza Kukamatwa Mkandarasi Na Mhandisi Mshauri Wa Mradi Wa Barabara Ya Kitunda–Kivule–Msongola

0
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI)

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Reuben Kwagilwa, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuwakamata na kuwahoji Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kitunda–Kivule–Msongola, kufuatia ucheleweshaji usioridhisha wa utekelezaji wa mradi huo.

Agizo hilo limetolewa baada ya Kwagilwa kufanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo, unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 30.37 na Kampuni ya Jiangxi Geo Engineering Co. Ltd, huku Mhandisi Mshauri wa mradi akiwa ni Mhandisi Consultancy Ltd. Hadi sasa, kiasi cha Shilingi bilioni 4 tayari kimeshalipwa kwa mkandarasi huyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kwagilwa amesema Serikali haitavumilia uzembe wala kutotekelezwa kwa mikataba kwa wakati, akisisitiza kuwa mradi huo ni muhimu kwa ustawi wa wananchi na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, ninakuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuhakikisha hawa wahusika wanakamatwa na kuhojiwa mara moja. Wanapaswa kutoa mpango wa utekelezaji wa mradi huu. Hakutakuwa na nyongeza ya muda hata kwa sekunde moja; mwezi wa nne mradi huu lazima uwe umekabidhiwa,” amesema Kwagilwa.

POLISI YATOA TAMKO ZITO KWA WATANZANIA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

Leave A Reply