Kwaya ya Gethsemane Ilivyoomboleza Kwenye Kumuaga Hayati Prof. Philemon Sarungi
Waimbaji wa Kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni GGK – SDA ya Jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za faraja wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Hayati Profesa Philemon Sarungi aliyefariki dunia Machi 5 mwaka huu. Mwili wa Profesa Sarungi umeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee Jijini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa, mawaziri wastaafu pamoja na wananchi.