The House of Favourite Newspapers

Lampard Atakiwa Chelsea Kuwa Kocha

SIKU za hesabu za kocha Maurizio Sarri zinahesabika baada ya kuibuka taarifa kuwa tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich anamtaka Frank Lampard ainoe timu hiyo.

 

Lampard ni staa wa zamani wa Chelsea, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wakati alipokuwa anawachezea kama kiungo mshambuliaji.

 

Sarri, hata hivyo, ana uwezekano mkubwa akaenda zake Juventus baada ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kumchukua.

 

Juventus wamepanga kutoa fidia ya pauni milioni tano kwa Chelsea ili waachiwe Sarri. Abramovich amevutiwa na kazi aliyofanya Lampard katika timu ya Derby County, ambayo anainoa. Lampard ameisaidia Derby kufika fainali ya mtoano wa Ligi Daraja la kwanza England ambapo watacheza dhidi ya Aston Villa kesho Jumatatu.

 

Abramovich anataka kumpa kazi hiyo Lampard asaidiane na kipa wa zamani wa Chelsea, Petr Cech, ambaye anaachana na Arsenal msimu huu baada ya kuamua kuachana na soka.

 

Hata hivyo, kuna wadau wa soka wanaona itakuwa mapema sana kwa Lampard kupewa kazi hiyo kwani ndio amemaliza msimu wake wa kwanza na Derby County. Juventus kwa upande wao wanasaka kocha mpya kufuatia kuondoka kwa Massimo Allegri

Comments are closed.