×

Messi Afunguka Sababu ya Kulia Baada ya Kufunga Hat-Trick Kombe la Dunia 2026

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, amefichua sababu iliyomfanya ashindwe kuzuia hisia zake na kulia baada ya kufunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Algeria kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026.

Messi, mwenye umri wa miaka 38, alionekana akifuta machozi kwa jezi yake mara baada ya kuifungia Argentina bao la kwanza katika mchezo huo uliochezwa mjini Kansas City. Baada ya mechi, nyota huyo alieleza kuwa machozi hayo hayakuhusiana na soka bali yalitokana na changamoto binafsi alizokuwa akipitia katika siku za hivi karibuni.

“Kwa nini nililia? Ilikuwa ni jambo ambalo halihusiani kabisa na mpira wa miguu. Nilipitia siku ngumu,” alisema Messi huku akiwashukuru wachezaji wenzake na viongozi wa timu kwa kumuunga mkono katika kipindi hicho kigumu.

Katika mchezo huo, Messi aliandika historia kwa kufunga hat-trick yake ya kwanza kabisa katika Kombe la Dunia, akiiwezesha Argentina kuanza vyema utetezi wa taji lao. Mabao hayo pia yalimfikisha jumla ya mabao 16 katika historia ya Kombe la Dunia, rekodi inayomfanya alingane na Miroslav Klose kama wafungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo.

Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, alimsifu Messi baada ya mchezo huo akisema: “Sina maneno kuhusu Leo. Ni wa kipekee.”

Familia ya Messi, ikiwemo mkewe Antonela Roccuzzo pamoja na watoto wao watatu, walikuwepo uwanjani kushuhudia usiku huo wa kihistoria ambao uliwaondoa pia mashabiki hofu kuhusu majeraha aliyokuwa nayo kabla ya mashindano kuanza.

Leave a Comment